Skip to main content

Usiyaone matatizo ya kiuchumi kama Kikwazo – Mwl Mwakasege


mwakasege

Shalom,

Tunajua unataka uwe na uchumi mzuri. Hii ni kwa mwanadamu yeyote bila kujali mahali alipo,awe anafanya kazi au hata kama hafanyi kazi.

Kuanzia leo na siku kadhaa zitakazofuata,tutajitahidi kukushirikisha misingi kadhaa iliyomo katika biblia,ambayo tunaamini itakusaidia uwe na uchumi mzuri. Msingi wa kwanza ni huu:Badilika unavyoamini juu ya uchumi,utabadilika unvyosema juu ya uchumi,na hali yako ya uchumi itabadilika vivyo hivyo.

Tunaamini ya kuwa; mtu akibadilika anavyoamini atabadilika pia anavyosema;na hali yake ya maisha itabadilika vivyo hivyo.
Jambo hili tunalipata tunaposoma kitabu cha Mithali 23:7 ya kuwa; “Maana aonavyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.”
Tafsiri nyingine ya mstari huu inasema;”maana awazavyo nafsini mwake ndivyo alivyo.” Tasfiri nyingine ya mstari huu inasema;”maana aaminivyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.” Mstari huu unataka tujue ya kuwa maisha ya mtu alivyo ni matokeo ya awazavyo au aaminivyo au afikirivyo(mindset), nafsini mwake.

Ulivyo kimaisha kwa nje ni matokeo ya msimamo wako wa kimawazo ndani yako. Kwa ulivyo kiuchumi,ni matokeo ya msimamo wako kimawazo(mindset),ulionao ndani yako juu ya uchumi.

Wapelelezi 10 walileta habari mbaya walipotoka kuipeleleza Kaanani,kwa vile waliamini mioyoni mwao ya kuwa “majitu” waliyoyakuta Kaanani yalikuwa kikwazo na pingamizi kwao.Wapelelezi wawili (Yoshua na Kalebu),waliona hayo “majitu” pia lakini mioyoni mwao waliamini tofauti. hawakuyaona majitu kama kikwazo bali waliyaona kama fursa kwao ya kutatua tatizo hilo ili waweze kula.

Soma habari hii katika kitabu cha hesabu 13:32,33 na Hesabu 14:9,28
Matokeo ya tofauti hizo kuwaza na kuamini,kuliamua hatma ya baadaye ya uchumi na maisha yao.Wapelelezi 10 waliishia kulalamika na kushindwa kwenda Kaanani. Na wale wawili (Yoshua na Kalebu) waliweza kwenda Kaanani na wakawa na maisha mazuri.

Wazo tunalokufikirisha siku hii ya leo ni kwamba;Usiyaone matatizo ya kiuchumi yanayokuzunguka kama kikwazo,bali yaone fursa ya kuyatatua ili iwe njia mojawapo ya kuongeza kipato chako. Kumbuka wanaolalamika wanapoona matatizo,wanajipofusha fikra szao wasiona fursa za kimaendeleo katika matatizo hayo.

Mungu awabariki.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA UIMBAJI NA MUZIKI

Uimbaji asili yake ni mbinguni (Eze 28:13-15). Tutakapofika mbinguni tutaendelea kumwimbia Bwana (Ufu 15:2-4; Ufu 5:9-10). Hapa duniani nyimbo na muziki vilianza zamani sana baada ya kuumbwa kwa Adamu na Hawa “…na jina la nduguye aliitwa Yubali; huyo ndiye baba yao wapigao kinubi na filimbi.”(Mwa 4:1-21). UMUHIMU WA KWAYA KATIKA KANISA Kwaya ni kikundi cha watu wanaoimba pamoja(na kupiga vyombo vya muziki). Kwaya ni kiungo muhimu katika Kanisa kinachofanya huduma ya uimbaji. Wapo wanakwaya wenye vipaji vya uimbaji, sauti za kuvutia na uwezo wa kutunga nyimbo mpya. Kanisa ni mwili wa Kristo wenye viungo vingi; na kila kiungo kina kazi. Kiungo hiki (Kwaya) kikitimiza vizuri wajibu wake, Kanisa litahudumiwa (1 Pet 4:10-11). Kwaya ni muhimu ndio maana hata katika Agano la Kale walikuwepo watu maalum waliowekwa kufanya huduma ya uimbaji (1Nya 6:31-32). Maneno ya nyimbo yana nguvu kubwa. Yanaweza kubadili hali ya huzuni kuwa ya furaha na moyo mgumu kuwa laini. Mtu mwenye udhaifu anaweza ku...

"UJUE ULIMWERNGU WA ROHO" na Mwl. Christopher Mwakasege

Ujue Ulimwengu wa roho. Kitabu kipya kilichotoka mwezi huu wakati wa semina ya Dar es salaam. Katika kitabu hiki utajifunza mambo mengi yanayohusu ulimwengu wa roho katika mpangilio wa sura kumi kama ifuatavyo; 1. Kufahamu umuhimu wa kujua uhalisi wa kuwepo kwa ulimwengu wa roho.  2. Kwa njia ya maombi unaweza kuwa mahali kiroho ambapo huwezi kuwa kimwili.  3. Mtu aliumbwa aishi katika maeneo mawili kwa wakati mmoja.  4. Mungu anakukaribisa katika ulimwengu wa roho ushiriki maamuzi pamoja naye kwa njia ya maombi yako.   5. Kufanikiwa kwako katika maombi kunategemea unavyoitunza na unavyoitumia nafasi yako uliyonaayo katika ulimwengu wa roho.  6. Tambua umuhimu wa nafasi unayoitumia unapomwomba Mungu.  7. Chanzo cha mamlaka uliyonayo katika ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi.  8. Umuhimu wa kujijua unajulikanaje katika ulimwengu wa Kiroho. 9. Inawezekana Mungu amejibu maombi yako ila yamekwama katika ulimwengu wa roho.  10. Kwa maombi ya...

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI EMMANUEL MGOGO KUFUNGA NDOA TARE 14 KATIKA KANISA LA EAGT IYUNGA MBEYA JUMAMOSI IJAYO

Emmanuel mgogo akiwa na mkewe mtarajiwa              TAZAMA VIDEO YA MSIKILIZE MUNGU YA EMMANUEL MGOGO. STORY,. Mwanamuziki nguli wa mziki wa injili anayetamba na albamu mbalimbali kama vile Ipo wapi njia ile,Msikilize mungu,na Usipotelee mwishoni hatimaye baada ya maisha ya upweke sasa amemsikiliza Mungu na tare 14 november mwaka huu anatarajia kufunga ndoa katika kanisa la eagt iyunga jijini Mbeya  akizungumza na mtandao huu Emmanuel Mgogo amesema mpaka sasa maandalizi yanaendelea vizuri hivyo anamwamini mungu kuwa ataifanikisha